Wednesday, July 27, 2011

MUUAJI WA NORWAY....ALIM-MIND STL TOKA KENYA...!

                                                         STELLA MWANGI AKA STL

Muuaji anayedaiwa kuua watu zaidi ya 90 toka Norway,Anders Behring Breivik inadaiwa kuwa hakupenda jinsi Rapper toka Kenya anayeishi Norway Stella Mwangi aka STL aliyeiwakilisha nchi ya Norway kwenye Eurovision contest May 14,2011 jamaa alitoa maneno makali kiaina kwa Stella Mwangi akifunguka; Nchi yangu haina maana kabisa,siasa zake hazijatulia inakuaje mzamiaji toka Kenya,tena anaimba bongo song analiwakilisha bara la Ulaya na nchi yangu? Bora Ujerumani washinde!

ANDERS BEHRING BREIVIK

STL alishiriki kwenye Melodi Grand Prix 2011 na kuiwakilisha nchi ya Norway kwenye Eurovision Song Contest 2011,iliyofanyika jijini Düsseldorf,Ujerumani February 2011,na mwezi May 2011 aliiwakilisha Norway kwenye fainali ya Eurovision Song Contest kupitia wimbo wake wa Haba Haba 

T-PAIN....AZINGUANA NA KAMPUNI YA AUTO TUNE?!

                                             FAHEEM NAJM AKA TALHASEE PAIN (T-PAIN)

Kuna mvutano wa kibiashara uliofikishwa kwenye vyombo vya sheria, kati ya Rapper na Producer,Faheem Najm aka T–Pain na Antares Technologies ambayo ambayo ilikua na mkataba na T-Pain ya matumizi ya Autotune affect
AUTO-TUNE EFFECT
  
T-Pain ambaye ni maarufu sana kwa kutumia Autotune effect,alimaliza mkataba na kampuni hiyo mwezi June na na kuanzisha kampuni iitwayo Izotope itakayo-promote audio effects za T-Pain ziitwazo The T-Pain Effect, na T-Pain alifungua mashitaka kwenye mahakama ya California akidai kuwa Kampuni ya Antares inaendelea kumtumia kwenye biashara ya bidhaa zake kama kawa,huku mkataba ukiwa umekwisha na pia itamuharibia biashara yake yenye teknolojia iitwayo I Am T-Pain Mic Kikubwa zaidi T-Pain anataka kampuni hiyo ya Antares iache kutumia picha,sauti au kitu chake chochote kwenye bidhaa zake 

UNAWEZA KUSEMA NI UTANI ILA NI KWELI KIMENUKA KIVU NCHINI CONGO

BINADAMU TUWE NA ULUMA KAMA FM ACADEMIA WALIVYOSEMA 

FAMILIA YA MICHAEL JACKSON....YATANGAZA SHOW...!

Show ya kumkumbuka King wa Pop duniani,Michael Joseph Jackson imepangwa kufanyika Mwezi October 2011 kwa mujibu wa familia yake

Mama yake MJ,Katherine ndugu zake LaToya,Tito,Marlon na Jackie walihudhuria press conference jijini Los Angeles kutangaza show hiyo ambayo imebatizwa jina la Michael Jackson Forever Tribute Concert ambayo itafanyika tarehe 8October kwenye uwanja wa Cardiff Millennium Stadium 

...               .FAMILIA YA MICHAEL JACKSON...PRESS CONFERENCE-LOS ANGELES....

Kwa sasa haijajulikana ni wasanii gani wata-perform na ila watatangazwa mwezi ujao na ticket zitaanza kuuzwa tarehe 3 August,2011 na sehemu ya mapato ya show hiyo yatapelekwa kwenye vituo kadhaa kikiwemo cha AIDS Project Los Angeles