Monday, August 29, 2011

WAJUE WAZEE WA ZAMANI

Wajue Fauvette
Marehemu Ndala Kasheba na King Kiki

                                        Maquis wakiwa katika show yao moja jijini Nairobi
Mbombo wa Mbomboka akifuatiwa na Adios, na mwisho Audax, kwa nyuma na Sax ni Mzee Chinyama


Visa alivyotenda Wallace mama
Sintovisahau, maishani mwangu,
Alinidanganya nihame kwetu, kisha anipe tabu mimi,
Halali nyumbani Wallace sijui yu wapi.
Chorus
Chakula nakula kwa jirani jama
Mafuta ya taa kwa jirani jama
Mwishowe jirani wamechoka jama
Kulala na lala peke yangu jama
Tabora Jazz Band 1969/70
Wallace kanifukuza nende kwetu

GADDAFI BADO TISHIO LIBYA


Kanali Muhamali Gaddafi
Msemaji wa kijeshi wa waasi Kanali Ahmed Omar Bani amesema watu wapatao elfu 50 waliokamatwa miezi ya karibuni hawajulikani walipo.
Waasi wanaamnini kuwa wafungwa hao huenda wanashikiliwa katika maghala ya kijeshi yaliyoko chini ya ardhi, ambayo yametelekezwa.
Vikundi vya kutetea haki za binadamu vina ushahidi kwamba watu wengi wameuawa karibu na magereza, lakini Kanali Bani hajamshutumu yeyote kwa mauaji ya wafungwa hao.
"Idadi ya watu waliokamatwa kwa miezi kadha iliyopita inakadiriwa kuwa kati ya 57,000 na 60,000," amesema katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Benghazi."Mpaka sasa, Kati ya wafungwa 10,000 na 11,000 wameachiliwa huru... wengine wako wapi?"
Kanali Bani ameomba kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu wafungwa hao kujitokeza, na amesema itakuwa jambo la kutisha iwapo wameuawa.
kuna hofu kuwa maelfu ya wateka wangali wanashikiliwa katika jela lililojengwa chini ya ardhi ambako inasaidikiwa kuwa wamekimbiwa na majeshi ya Kanali Gaddafi wakati waasi walipoingia Tripoli na kuuteka nyara.
Kinachoendelea kwa wakati huu ni pilka pilka za kuwatafuta mateka hao ambao hawajulikano waliko ili waachwe huru.
Al-Megrahi
wakati huo huo viongozi waasi wamesema hawana nia yakumrudisha Abdel Basset al-Megrahi ambaye mwaka 1988 alifungwa jela kwa kulipuwa ndege ya Lockerbie katika anga ya Scotland.
Megrahi aliachiliwa mapema kutika jela miaka miwili iliyopita baada ya madaktari kudai anakaribia kufariki kwani ana miezi michache tu ya kuishi . kuachiliwa kwake kulipingwa na wengi.
Lakini hivi majuzi kumekuwa na shinikozo za kumtaka Megrahi arudishwe uingereza au akafunguliwe amshitaka upya nchini Marekani.
Na shirika la harabi la CNN limemkuta bwana huyo katika jumba la kifahari viungani mwa mji wa Tripoli lakini akiwa mahututi chini ya uangalizi wa familia yake.

TAARIFA YA BAKWATA KUHUSU EID AL-FITRI 2011

YAH: EID-EL FITRI, AGOSTI, 2011 

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linapenda kuwatangazia waislam na wananchi kwa ujumla kuwa suala ya EId- El Fitri kwa mwaka 2011, itaswaliwa kitaifa katika msikiti wa masjid Gaddaf-Mjini Dodoma mnamo tarehe 30 au 31 Agosti 2011, kutegemeana na muandamo wa mwezi.

Aidha baraza la EId- El Fitri, litafanyika siku hiyo hiyo na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi wa Jamuhuri ya muuungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Lilwete.

Ujumbe wa mwaka huu wa EId-El Fitri ni “wazazi wawalee watoto wao kwa mujibu wa mafundisho ya kiislam”. Uongozi wa Baraza kuu la waislam wa Tanzania (BAKWATA) linapenda kuwatakia waislam na watanzania kwa ujumla sikukuu njema, na Ishallah, tusheherekee kwa amani na upendo.

EID MUBARAKA.

Shabani Simba.
Meneja Mawasiliano (BAKWATA H/O).

Kwa mawasiliano zaidi piga namba ifuatayo
Cell: 0656 315997 Au 0755360745. 


source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/08/taarifa-ya-bakwata-kuhusu-eid-el-fitr-2011.html#ixzz1WUFkWkZq

MAPOROMOKO UGANDA YAZIDI KUUA WATU



Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo mashariki mwa Uganda imepanda na kufikia watu 35, huku Watu wawili wakifariki dunia katika wilaya ya Bulambuli baada ya makumi ya wengine kufariki dunia hapo jana.

Hadi kufikia sasa waokoaji wamefanikiwa kupata miili 24 ingawa inaaminika kuwa takriban watu 35 wameuawa kwenye janga hilo la kimaumbile.

Mwaka uliopita mamia ya watu walifariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo katika maeneo ya Mlima Elgon na serikali ikaahidi kuwa ingewahamisha wakaazi katika maeneo ambayo hukumbwa na majanga kama hayo lakini haikutekeleza ahadi hiyo.

Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu pamoja na maafisa wa polisi wanaendelea na shughuli za uokoaji nchini humo.

MPIGIE KURA MREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA

SMS Mrembo 1 kwenda 15550 SMS Mrembo 2 kwenda 15550


                                  SMS Mrembo 3 kwenda 15550 SMS Mrembo 4 kwenda 15550

SMS Mrembo 5 kwenda 15550 SMS Mrembo 6 kwenda 15550


SMS Mrembo 10 kwenda 15550 SMS Mrembo 11 kwenda 15550


SMS Mrembo 12 kwenda 15550: SMS Mrembo 14 kwenda 15550

IDD EL FITR


Idd el Fitr (Kiarabuعيد الفطر ‘idu l-fiṭr; pia: Eid ul-FitrId-Ul-FitrIddul FitriIddi al Fitr) ni sikukuu ya kiislamu inayomaliza mwezi wa Ramadan. Kipindi cha kufunga kinamalizika kwenye sikukuu hiyo. Ni sherehe ya siku tatu.
Idd el Fitr inaanza mara mwezi wa hilali umeonekana baada ya Ramadan.
Waislamu huvaa nguo safi mara nyingi nguo mpya na kutoa zawadi kwa maskini. Misikiti na nyumba mara nyingi zimepambwa. Ni nafasi ya kufurahia kati ya Waislamu.
 (Kiarabuعيد الفطر ‘idu l-fiṭr; pia: Eid ul-FitrId-Ul-FitrIddul FitriIddi al Fitr) ni sikukuu ya kiislamu inayomaliza mwezi wa Ramadan. Kipindi cha kufunga kinamalizika kwenye sikukuu hiyo. Ni sherehe ya siku tatu.
Idd el Fitr inaanza mara mwezi wa hilali umeonekana baada ya Ramadan.
Waislamu huvaa nguo safi mara nyingi nguo mpya na kutoa zawadi kwa maskini. Misikiti na nyumba mara nyingi zimepambwa. Ni nafasi ya kufurahia kati ya Waislamu.