Friday, August 12, 2011

CHUO KIKUU CHAFUNGWA SWAZILAND


Chuo hicho kimetangaza kuwa hatua ya kusajili imesimamishwa na masomo kuahirishwa. Kiongozi wa jumuiya ya wanafunzi Pasika Dlamini alisema wanafunzi wengi hawakuhudhuria masomo baada ya tangazo hilo.

Nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa fedha kiasi ambacho wiki iliyopita Afrika Kusini iliamua kuwapa mkopo wa dharura wa dola za kimarekani milioni 355 na tayari chuo hicho kimethibitisha kuwa fedha bado hazijafika kuwalipia ada wengi wa wanafunzi hao, hakikuweza kufunguliwa. " Tuliambiwa kuwa chuo hakitafunguliwa siku ya Jumatatu, kwasababu hamna pesa
 

 Chuo kikuu cha Swaziland hakijafunguliwa kwa mwaka mpya wa masomo baada ya serikali kushindwa kutoa fedha za ada za wanafunzi.
Mwaka huu serikali ilisema itawafadhili takriban wanafunzi 300, kiwango kilichopungua sana ukilinganisha na wanafunzi 1,200 mwaka jana. Mapato ya Swaziland ya mwaka jana kutoka ushuru wa forodha wa kusini mwa Afrika- chanzo kikuu cha fedha nchini humo- kilishuka kwa asilimia 60.

Baada ya kukubaliana na mkopo, Afrika Kusini ilisistiza jirani yake mdogo lazima ifanye mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa. Mfalme Mswati III, mfalme pekee barani Afrika mwenye mamlaka kamili, ameshutumiwa kwa kuishi kwa ufahari na wake zake 13, huku watu wake wengi wakibaki maskini.

Pia kumekuwa na ripoti kuwa nchi hiyo, ambayo ina waathiriwa wengi wa virusi vya ukimwi dunaini, imepungukiwa na dawa za kufubaza ukimwi za ARV.
 

DR. Shein kuzindua ZANZIBAR ya kwanza ya fasihi na Jazz Festival

President Ali Mohamed Shein will launch Zanzibar’s first international literary and jazz festival at world heritage site - Stone Town (Zanzibar) - on 2 September.

Zanzibar’s President will be opening the ‘Jahazi Literary and Jazz Festival’ at an official ceremony held in the Old Fort alongside the former United Nations Deputy Secretary-General, Lord Malloch Brown.

The President said: “I believe this festival will raise awareness on importance of people’s culture, democracy, respect for human rightsand better management of Africa’s resources.”
 


SERIKALI YAIFUNGIA BP MIEZI MITATU


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamko la Serikali la kuifungia Kampuni ya BP, kwa miezi mitatu kwa kutotimiza agizo la kuacha mgomo wa kuuza mafuta. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)