Saturday, July 30, 2011

FC Barcelona Vs Manchester United mechi ya itakayochezwa ndani ya FedEx Landover MD


Kwawale wapenzI wote wa mpira wa migu, kutakuwa kizaza cha mechi ya kimataifa baina ya mapingwa wa ulaya FC Barcelona vs Manchester United, itakayochezwa siku ya Jumamosi Julai 30, mida ya saa 7:00 katika kiwanja cha FedEx Landover, Maryland 20785. 

Msanii wa hip hop nchini Marekani Ludacris awasali Tanzania

Msanii wa hip hop nchini Marekani na muigizaji filamu Brian Christopher Bridges pak Ludacris awasali Tanzania kwa ajili ya kuonyesha maadhimisho ya miaka kumi ya Serengeti Fiesta 2011 kufanyika siku ya jumamosi Julai 30 katika viwanja Viongozi Club, Kinondoni, Dar es Salaam. 


Mwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk Kilimanjaro jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onyesho lake moja ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar. 

WANAFUNZO WA SKULI YA SEKONDARI YA VIKOKOTONI WAKIUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHANI

SHEKH Mselemu Ali akitowa mhadhara kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni kwa ajili ya kutowa mafunzo ya Mfungo wa Ramadhani, unaotarajiwa kuaza mwazoni mwa mwezi wa Nane. 

WANAFUNZI wa Skuli ya Vikokotoni wakimsikiliza Shekh. Mselem Ali akitowa mawaidha ya dini ya Kiislam kwa Wanafunzi hao ikiwa ni moja ya Maandalizi ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutowa mafunzo ya dini, mdahalo huo umeandaliwa na Uongozi wa skuli hiyo uliofanyika katika viwanja vyao. 


MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA OMAN


Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif Hamad alipokuwa katika mazungumzo na Balozi mdogo wa Omananayemaliza muda wake Majid Abdulla Al Abbad Ofisini kwake Migombani.

Na Abdi Shamnah –OMKR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim seif Sharif Hamad amesema kuwa ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman umeimairika sana katika kipindi cha miaka sita, kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na Balozi mdogo wa nchi hiyo hapa nchini, Majid Abdulla Al –Abbad, ambae amemaliza muda wake.


Maalim Seif amesema hayo leo ofisini kwake Migombani alipokutana na Balozi huyo anaerudi nyumbani baada ya kuitumikia nchi yake kwa kipindi cha miaka sita. 

Seneti imepinga mswada wa deni Marekani

Baraza la seneti linalodhibitiwa na chama cha Democratic nchini Marekani liliupinga mswada wa kupandisha kiwango cha ukopaji wa serikali kupitia kura 59 dhidi ya 41

Hii ni baada ya baraza la wawakilishi nchini Marekani limeidhinisha pendekezo la chama cha Republican, kupandisha kiwango cha ukopaji cha nchi hiyo katika awamu mbili, kupitia kura 218 dhidi ya 210. 


Spika wa bunge John Boehner 

Baadhi ya wanachama wa Republican walijiunga na wale wa Democratic kupinga hatua hiyo ya wabunge wenzao.

Wasiwasi ulizidi kufuatia kuwadia siku ya Ijumanne ambayo wizara ya fedha ya Marekani inasema ndio siku ya mwisho kuwa na akiba ya kutosha ili kuweza kutekeleza wajibu wake wa kuwalipa wamiliki wa hisa za serikali pamoja na wastaafu, maskini, na wale wanaohitaji huduma za afya.

Spika wa bunge John Boehner aliahirisha kura hiyo kwa siku mbili, akibishana na wanachama wenzake katika jitahada ya kuwashawishi kuunga mkono mpango huo.