Saturday, July 30, 2011

Seneti imepinga mswada wa deni Marekani

Baraza la seneti linalodhibitiwa na chama cha Democratic nchini Marekani liliupinga mswada wa kupandisha kiwango cha ukopaji wa serikali kupitia kura 59 dhidi ya 41

Hii ni baada ya baraza la wawakilishi nchini Marekani limeidhinisha pendekezo la chama cha Republican, kupandisha kiwango cha ukopaji cha nchi hiyo katika awamu mbili, kupitia kura 218 dhidi ya 210. 


Spika wa bunge John Boehner 

Baadhi ya wanachama wa Republican walijiunga na wale wa Democratic kupinga hatua hiyo ya wabunge wenzao.

Wasiwasi ulizidi kufuatia kuwadia siku ya Ijumanne ambayo wizara ya fedha ya Marekani inasema ndio siku ya mwisho kuwa na akiba ya kutosha ili kuweza kutekeleza wajibu wake wa kuwalipa wamiliki wa hisa za serikali pamoja na wastaafu, maskini, na wale wanaohitaji huduma za afya.

Spika wa bunge John Boehner aliahirisha kura hiyo kwa siku mbili, akibishana na wanachama wenzake katika jitahada ya kuwashawishi kuunga mkono mpango huo. 

No comments: