Saturday, July 30, 2011

MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA OMAN


Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif Hamad alipokuwa katika mazungumzo na Balozi mdogo wa Omananayemaliza muda wake Majid Abdulla Al Abbad Ofisini kwake Migombani.

Na Abdi Shamnah –OMKR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim seif Sharif Hamad amesema kuwa ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman umeimairika sana katika kipindi cha miaka sita, kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na Balozi mdogo wa nchi hiyo hapa nchini, Majid Abdulla Al –Abbad, ambae amemaliza muda wake.


Maalim Seif amesema hayo leo ofisini kwake Migombani alipokutana na Balozi huyo anaerudi nyumbani baada ya kuitumikia nchi yake kwa kipindi cha miaka sita. 

No comments: