Monday, September 19, 2011

Wanafunzi wa Royal College wachangia damu

Wizara ya Afya kupitia mfuko maalum wa kuchangisha Damu salama, leo umetembelea katika chuo cha Uandishi na Utangazaji cha Royal Tanzania College kwaajili ya kutoa elimu na kuchangisha damu.

Wanafunzi wa cho hicho waliweza kupata elimu kutoka kwa mwakilishi wa damu salama ambaye ali;kuja hapo ndugu Joseph na baadaye kujiunga na Staff wa chuo hicho kwaajili ya kutoa damu hiyo.

Miongoni mwa faida ambazo mtu anapotoa damu ni kusaidia watu ambao huenda wangefariki kutokana na kukosa damu, ikiwemo waliopata ajali, wanaojifungua na wenye magonjwa mbalimbali ambayo wanahitaji damu. pia alisema kwamba mtu anapotoa damu huwa anajijua kama yupo group gani la damu, hivyo ni rahisi kwakwe kupata huduma ya damu pindi inapohitaji hivyo kwakuwa anakuwa anajulikana yeye ni group gani. pia amesema mtu huweza kujua afya yake kwakuwa hupima afya bule, bila ya hata gharama wakati hospitalini huwa gharama kubwa kuangalia afya. mwisho mwanachama hupewa kitambulisho cha uanachama ambacho kitakuwa kikimsaidia yeye na familia yake, ingawa hata kama sio mwanachama utapewa damu lakini wewe huwa unajulikana kitaifa kama ni mchangia damu.


Principle wa Cho aliyekaa chini Mr Omary Bahari na

Msimamizi akieleza jinsi ya kuchangia damu, alisema anachunguza, afya, wingi wa damu, magonjwa ya kuambukiza na umri wa mtu anayetakiwa kutoa damu lazima uzidi miaka kumi na nane.