YAH: EID-EL FITRI, AGOSTI, 2011
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linapenda kuwatangazia waislam na wananchi kwa ujumla kuwa suala ya EId- El Fitri kwa mwaka 2011, itaswaliwa kitaifa katika msikiti wa masjid Gaddaf-Mjini Dodoma mnamo tarehe 30 au 31 Agosti 2011, kutegemeana na muandamo wa mwezi.
Aidha baraza la EId- El Fitri, litafanyika siku hiyo hiyo na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi wa Jamuhuri ya muuungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Lilwete.
Ujumbe wa mwaka huu wa EId-El Fitri ni “wazazi wawalee watoto wao kwa mujibu wa mafundisho ya kiislam”. Uongozi wa Baraza kuu la waislam wa Tanzania (BAKWATA) linapenda kuwatakia waislam na watanzania kwa ujumla sikukuu njema, na Ishallah, tusheherekee kwa amani na upendo.
EID MUBARAKA.
Shabani Simba.
Meneja Mawasiliano (BAKWATA H/O).
Kwa mawasiliano zaidi piga namba ifuatayo
Cell: 0656 315997 Au 0755360745.
source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/08/taarifa-ya-bakwata-kuhusu-eid-el-fitr-2011.html#ixzz1WUFkWkZq
No comments:
Post a Comment