Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo mashariki mwa Uganda imepanda na kufikia watu 35, huku Watu wawili wakifariki dunia katika wilaya ya Bulambuli baada ya makumi ya wengine kufariki dunia hapo jana.
Hadi kufikia sasa waokoaji wamefanikiwa kupata miili 24 ingawa inaaminika kuwa takriban watu 35 wameuawa kwenye janga hilo la kimaumbile.
Mwaka uliopita mamia ya watu walifariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo katika maeneo ya Mlima Elgon na serikali ikaahidi kuwa ingewahamisha wakaazi katika maeneo ambayo hukumbwa na majanga kama hayo lakini haikutekeleza ahadi hiyo.
Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu pamoja na maafisa wa polisi wanaendelea na shughuli za uokoaji nchini humo.
No comments:
Post a Comment