Monday, July 25, 2011

UN yaomba ulimwengu utoe michango ya dharura kwa Pembe ya Afrika

                                         Jacques Diouf,Mkurugenzi
                                                 mkuu wa FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, limeutolea wito ulimwengu mzima kufanya kila linalowezekana kuchukua hatua za kuliokoa eneo la Pembe ya Afrika linalokumbwa na baa kubwa la njaa na ukame.

Kauli hizo zimetolewa katika kikao cha dharura cha FAO kilichoandaliwa mahsusi kwasababu ya tatizo hilo. Kulingana na takwimu rasmi, kiasi ya Wasomali milioni 3.7 wanakabiliwa na kitisho cha njaa. Ifahamike kuwa njaa ukame umeliathiri eneo la Pembe ya Afrika zikiwemo nchi za Ethiopia na Kenya.

Kauli hizo zimetolewa katika kikao cha dharura cha FAO kilichoandaliwa mahsusi kwasababu ya tatizo hilo. Kulingana na takwimu rasmi, kiasi ya Wasomali milioni 3.7 wanakabiliwa na kitisho cha njaa. Ifahamike kuwa njaa ukame umeliathiri eneo la Pembe ya Afrika zikiwemo nchi za Ethiopia na Kenya.

Hali ni mbaya

 Akizungumza katika ufunguzi rasmi wa kikao hicho cha dharura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula, FAO, Jacques Diouf, alisema kuwa hali ni mbaya na hatua za dharura zinahitajika ili kuwanusuru wakaazi wa eneo hilo la Pembe ya Afrika.

Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi kuwa maeneo mawili ya Somalia yanakabiliwa na njaa. Ifahamike kuwa maeneo hayo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Al Shabaab wanaoaminika kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia aliye pia Waziri wa Mambo ya Nje alikihudhuria kikao cha leo, Mohamud Ibrahim anaelezea kuwa,

"Wasomali wanakabiliwa na njaa kwasababu kadhaa ikiwemo mvua chache kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, harakati za kundi la Al Shabaab zilizoweka amri ya kuyazuia mashirika ya msaada kusambaza vyakula, pamoja na usalama duni katika eneo hili.

No comments: