Saturday, July 30, 2011

FC Barcelona Vs Manchester United mechi ya itakayochezwa ndani ya FedEx Landover MD


Kwawale wapenzI wote wa mpira wa migu, kutakuwa kizaza cha mechi ya kimataifa baina ya mapingwa wa ulaya FC Barcelona vs Manchester United, itakayochezwa siku ya Jumamosi Julai 30, mida ya saa 7:00 katika kiwanja cha FedEx Landover, Maryland 20785. 

Msanii wa hip hop nchini Marekani Ludacris awasali Tanzania

Msanii wa hip hop nchini Marekani na muigizaji filamu Brian Christopher Bridges pak Ludacris awasali Tanzania kwa ajili ya kuonyesha maadhimisho ya miaka kumi ya Serengeti Fiesta 2011 kufanyika siku ya jumamosi Julai 30 katika viwanja Viongozi Club, Kinondoni, Dar es Salaam. 


Mwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk Kilimanjaro jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onyesho lake moja ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar. 

WANAFUNZO WA SKULI YA SEKONDARI YA VIKOKOTONI WAKIUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHANI

SHEKH Mselemu Ali akitowa mhadhara kwa Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni kwa ajili ya kutowa mafunzo ya Mfungo wa Ramadhani, unaotarajiwa kuaza mwazoni mwa mwezi wa Nane. 

WANAFUNZI wa Skuli ya Vikokotoni wakimsikiliza Shekh. Mselem Ali akitowa mawaidha ya dini ya Kiislam kwa Wanafunzi hao ikiwa ni moja ya Maandalizi ya kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutowa mafunzo ya dini, mdahalo huo umeandaliwa na Uongozi wa skuli hiyo uliofanyika katika viwanja vyao. 


MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA OMAN


Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif Hamad alipokuwa katika mazungumzo na Balozi mdogo wa Omananayemaliza muda wake Majid Abdulla Al Abbad Ofisini kwake Migombani.

Na Abdi Shamnah –OMKR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim seif Sharif Hamad amesema kuwa ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman umeimairika sana katika kipindi cha miaka sita, kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na Balozi mdogo wa nchi hiyo hapa nchini, Majid Abdulla Al –Abbad, ambae amemaliza muda wake.


Maalim Seif amesema hayo leo ofisini kwake Migombani alipokutana na Balozi huyo anaerudi nyumbani baada ya kuitumikia nchi yake kwa kipindi cha miaka sita. 

Seneti imepinga mswada wa deni Marekani

Baraza la seneti linalodhibitiwa na chama cha Democratic nchini Marekani liliupinga mswada wa kupandisha kiwango cha ukopaji wa serikali kupitia kura 59 dhidi ya 41

Hii ni baada ya baraza la wawakilishi nchini Marekani limeidhinisha pendekezo la chama cha Republican, kupandisha kiwango cha ukopaji cha nchi hiyo katika awamu mbili, kupitia kura 218 dhidi ya 210. 


Spika wa bunge John Boehner 

Baadhi ya wanachama wa Republican walijiunga na wale wa Democratic kupinga hatua hiyo ya wabunge wenzao.

Wasiwasi ulizidi kufuatia kuwadia siku ya Ijumanne ambayo wizara ya fedha ya Marekani inasema ndio siku ya mwisho kuwa na akiba ya kutosha ili kuweza kutekeleza wajibu wake wa kuwalipa wamiliki wa hisa za serikali pamoja na wastaafu, maskini, na wale wanaohitaji huduma za afya.

Spika wa bunge John Boehner aliahirisha kura hiyo kwa siku mbili, akibishana na wanachama wenzake katika jitahada ya kuwashawishi kuunga mkono mpango huo. 

Thursday, July 28, 2011

TUSKER ALL STARS


Tusker Project Fame's Tusker All Stars 2011 sees Hemedi Suleiman [TPF2] and another Tanzanian fan-favorite Peter Msechu [TPF4] both selected to join TAS. Uganda's Davis Ntare [TPF4 Winner] and dance-diva Caroline Nabulime[TPF3] also joined the star-studded cast of contestants. Kenyan contestants of 2011's TPF will be Amileena Mwenesi [TPF4], Bernard Ng'ang'a 'Ng'ang'alito' [TPF3] and Patricia Kihoro [TPF3]. Rwanda's Alpha Rwirangira [TPF3 Winner] will also be joining Tusker Project Fame 2011. 

WATUMIAJI MILIONI 7.5 WA FACEBOOK...UNDER 13 YRS...!

Utafiti umeonesha kuwa watumiaji milioni 7.5 kati ya milioni 20 millioni wa Facebook kwa mwaka jana wana umri wa miaka 13,na milioni 1 wametishiwa,kunyanyaswa kwa kutumia mtandao huo

Pia watumiaji milioni 5 wa Facebook wana miaka 10 zaidi au chini ya hapo,wanatumia mtandao huo bila ya ruhusa ya wazazi wao huku masharti ya kujiunga na mtandao huo wa Facebook unashauri angalau mtumiaji awe na miaka 13 lakini inasemekana kuwa wazazi wengi wanawapa vyeti feki vya kuzaliwa wakitaka ku-sign up kujiunga na mtandao huo 

WABUNGE CHADEMA....WATOLEWA BUNGENI LEO...!

MH GODBLESS LEMA - ARUSHA MJINI 

 Wabunge watatu toka Chama cha CHADEMA wametolewa nje ya ukumbi wa Bunge leo mchana na Naibu Spika,Job Ndugai...

MH TUNDU LISSU - SINGIDA MASHARIKI

                                                 MH PETER MSIGWA - IRINGA MJINI
Mbunge wa Arusha-Mjini,Mh GodBless Lema,Mbunge wa Iringa-Mjini Mh Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Singida-Mashariki,Mh Tundu Lissu walitolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa utovu wa nidhamu baada ya kuongea bila ya ruhusa ya Naibu Spika....

NANI KASEMA KUWA OFISINI WATU HUWA HAWALALI JE KAMA KAFANYA SANA KAZI


Jamaaa kauchapa usingizini ofisini 

luka katika pozi za ofisini 

KIKAO CHA WANACHAMA WA CONTRACTOR OF TANZANIA*CATA*

Wakwanza kushoto ni Kaimu Mwenyekiti Gaitan na katibu Bw, Nathani wakiongoza kikao cha wakandarasi mkoani Iringa.



Baadhi ya Wajumbe wa chama cha makandarasi na wamwisho kushoto ni Meneja wa Saccos ya CATA Mkoani Iringa. 


wajumbe wapo makini na mada zinazojadiliwa  

wakitafakari mada zijadiliwazo kuwa zinamanufaa. 


DAVID BECKHAM....ATOA YA MOYONI KUHUSU SOMALIA...!

Mwanasoka wa England,David Joseph Beckham ambaye ni Unicef Goodwill Ambassador ameandika ujumbe wenye masikitiko wa kuomba msaada kwa wanaokabiliwa na baa la njaa,hasa watoto nchini Somalia.... 



Beckham alifunguka toka chini ya mvungu wa moyo wake kuwa “Watoto wapatao milioni 2 toka Somalia wanakabiliwa na njaa na kila baada ya dakika 6 mtoto mmoja anafariki kutokana na njaa na kufunguka zaidi kuwa hapendi kuona watoto wake Brooklyn, Romeo,Cruz au Harper aende kulala bila ya kula sembuse mtoto mwingine na kutoa ujumbe “They need our help....They need our attention....They need our action” 


Wednesday, July 27, 2011

MUUAJI WA NORWAY....ALIM-MIND STL TOKA KENYA...!

                                                         STELLA MWANGI AKA STL

Muuaji anayedaiwa kuua watu zaidi ya 90 toka Norway,Anders Behring Breivik inadaiwa kuwa hakupenda jinsi Rapper toka Kenya anayeishi Norway Stella Mwangi aka STL aliyeiwakilisha nchi ya Norway kwenye Eurovision contest May 14,2011 jamaa alitoa maneno makali kiaina kwa Stella Mwangi akifunguka; Nchi yangu haina maana kabisa,siasa zake hazijatulia inakuaje mzamiaji toka Kenya,tena anaimba bongo song analiwakilisha bara la Ulaya na nchi yangu? Bora Ujerumani washinde!

ANDERS BEHRING BREIVIK

STL alishiriki kwenye Melodi Grand Prix 2011 na kuiwakilisha nchi ya Norway kwenye Eurovision Song Contest 2011,iliyofanyika jijini Düsseldorf,Ujerumani February 2011,na mwezi May 2011 aliiwakilisha Norway kwenye fainali ya Eurovision Song Contest kupitia wimbo wake wa Haba Haba 

T-PAIN....AZINGUANA NA KAMPUNI YA AUTO TUNE?!

                                             FAHEEM NAJM AKA TALHASEE PAIN (T-PAIN)

Kuna mvutano wa kibiashara uliofikishwa kwenye vyombo vya sheria, kati ya Rapper na Producer,Faheem Najm aka T–Pain na Antares Technologies ambayo ambayo ilikua na mkataba na T-Pain ya matumizi ya Autotune affect
AUTO-TUNE EFFECT
  
T-Pain ambaye ni maarufu sana kwa kutumia Autotune effect,alimaliza mkataba na kampuni hiyo mwezi June na na kuanzisha kampuni iitwayo Izotope itakayo-promote audio effects za T-Pain ziitwazo The T-Pain Effect, na T-Pain alifungua mashitaka kwenye mahakama ya California akidai kuwa Kampuni ya Antares inaendelea kumtumia kwenye biashara ya bidhaa zake kama kawa,huku mkataba ukiwa umekwisha na pia itamuharibia biashara yake yenye teknolojia iitwayo I Am T-Pain Mic Kikubwa zaidi T-Pain anataka kampuni hiyo ya Antares iache kutumia picha,sauti au kitu chake chochote kwenye bidhaa zake 

UNAWEZA KUSEMA NI UTANI ILA NI KWELI KIMENUKA KIVU NCHINI CONGO

BINADAMU TUWE NA ULUMA KAMA FM ACADEMIA WALIVYOSEMA 

FAMILIA YA MICHAEL JACKSON....YATANGAZA SHOW...!

Show ya kumkumbuka King wa Pop duniani,Michael Joseph Jackson imepangwa kufanyika Mwezi October 2011 kwa mujibu wa familia yake

Mama yake MJ,Katherine ndugu zake LaToya,Tito,Marlon na Jackie walihudhuria press conference jijini Los Angeles kutangaza show hiyo ambayo imebatizwa jina la Michael Jackson Forever Tribute Concert ambayo itafanyika tarehe 8October kwenye uwanja wa Cardiff Millennium Stadium 

...               .FAMILIA YA MICHAEL JACKSON...PRESS CONFERENCE-LOS ANGELES....

Kwa sasa haijajulikana ni wasanii gani wata-perform na ila watatangazwa mwezi ujao na ticket zitaanza kuuzwa tarehe 3 August,2011 na sehemu ya mapato ya show hiyo yatapelekwa kwenye vituo kadhaa kikiwemo cha AIDS Project Los Angeles

Tuesday, July 26, 2011

Kikao cha FAO chaanza rasmi mahsusi kwa eneo la Pembe ya Afrika

Ukame uliokithiri: Mifugo yafa kwa wingi na njaa imesambaa Ethiopia 

Ukame mbaya umelikumba eneo la Pembe ya Afrika na kusababisha tishio kubwa la njaa pia nchini Ethiopia. Wakati huo huo juhudi za kuyaokoa maisha ya mamilioni ya watu zitaimarishwa kwenye kikao cha FAO. 


Wajumbe wa serikali, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na wa mashirika ya misaada leo wanakutana mjini Rome kwa ajili ya kikao cha dharura kulijadili baa la njaa kwenye eneo la Pembe ya Afrika. Wajumbe kwenye kikao hicho wanazungumzia njia za kuwasaidia watu wapatao milioni 12 waliomo katika hatari ya kufa njaa.

Kikao hicho kinafanyika kufuatia shinikizo la kimataifa kuwataka viongozi wa dunia waongeze misaada kwa ajili ya mamilioni ya watu wanaotishiwa na baa la njaa lilisosababishwa na ukame mbaya ambao haujawahi kuonekana katika historia ya miaka 60 iliyopita katika eneo la Pembe ya Afrika. 

Marekani na Israel zalaumiwa kwa kukwamisha umoja wa kitaifa Palestina


Kiongozi mmoja wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ameilaumu Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kukwamisha ufanikishaji wa vipengee vya makubaliano ya umoja wa kitaifa Palestina.

Abu Ali Shakib, mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema kuwa, mchakato wa kuelekea kwenye umoja wa kitaifa ulioingia kasi kubwa baada ya kufikiwa makubaliano kati ya HAMAS na Fat'h umewatia hofu mabeberu wa dunia wakiongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni kiasi kwamba Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa akiingilia waziwazi mapatano hayo kupitia kumshinikiza Mahmoud Abbas na serikali yake kujiweka mbali na HAMAS.

Huku hayo yakiripotiwa, Salam Fayyadh, Waziri Mkuu wa serikali ya Mahmoud Abbas amesema kuwa, yuko tayari kujiuzulu nafasi yake ili kurahisisha utekelezaji wa makubalino ya umoja wa kitaifa ya Palestina.

Fayyadh amesema hayo alipohojiwa na televisheni ya serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Matamshi hayo ya Salam Fayyadh yamekuja baada ya kuongezeka mashinikizo na lawama dhidi yake kutokana na kukubali kuburuzwa na madola ya kigeni ikiwemo Marekani.


Monday, July 25, 2011

Pinda akiwa na wanafunzi wa CANADA



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na wanafunzi kutoka Canada ambao walishiriki katika kuchangisha fedha na kujenga kisima katika kitongoji cha Nyerere, Msalato, Dodoma. Alikuwa katika mkutano wa uzinduzi wa kisima hicho Julai 23,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Ludacris Ku-perform Tanzania July 30..!!!


  
Ludacris kutinga ndani ya Bongo dar es salaam kuwachizisha wa bongo na mizuka yao.

 Serengeti Fiesta 2011, Itachukua Nafasi a Julai 30.
Tukio hilo, litafanyika katika viwanja vya LEADERS CLUB, Kinondoni, Dar es Salaam.
So wabongo walabata kaa mkao wa kula na Ludacriss 

 







UN yaomba ulimwengu utoe michango ya dharura kwa Pembe ya Afrika

                                         Jacques Diouf,Mkurugenzi
                                                 mkuu wa FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, limeutolea wito ulimwengu mzima kufanya kila linalowezekana kuchukua hatua za kuliokoa eneo la Pembe ya Afrika linalokumbwa na baa kubwa la njaa na ukame.

Kauli hizo zimetolewa katika kikao cha dharura cha FAO kilichoandaliwa mahsusi kwasababu ya tatizo hilo. Kulingana na takwimu rasmi, kiasi ya Wasomali milioni 3.7 wanakabiliwa na kitisho cha njaa. Ifahamike kuwa njaa ukame umeliathiri eneo la Pembe ya Afrika zikiwemo nchi za Ethiopia na Kenya.

Kauli hizo zimetolewa katika kikao cha dharura cha FAO kilichoandaliwa mahsusi kwasababu ya tatizo hilo. Kulingana na takwimu rasmi, kiasi ya Wasomali milioni 3.7 wanakabiliwa na kitisho cha njaa. Ifahamike kuwa njaa ukame umeliathiri eneo la Pembe ya Afrika zikiwemo nchi za Ethiopia na Kenya.

Hali ni mbaya

 Akizungumza katika ufunguzi rasmi wa kikao hicho cha dharura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula, FAO, Jacques Diouf, alisema kuwa hali ni mbaya na hatua za dharura zinahitajika ili kuwanusuru wakaazi wa eneo hilo la Pembe ya Afrika.

Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi kuwa maeneo mawili ya Somalia yanakabiliwa na njaa. Ifahamike kuwa maeneo hayo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa Al Shabaab wanaoaminika kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia aliye pia Waziri wa Mambo ya Nje alikihudhuria kikao cha leo, Mohamud Ibrahim anaelezea kuwa,

"Wasomali wanakabiliwa na njaa kwasababu kadhaa ikiwemo mvua chache kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, harakati za kundi la Al Shabaab zilizoweka amri ya kuyazuia mashirika ya msaada kusambaza vyakula, pamoja na usalama duni katika eneo hili.

Shukurani za Sara Baby Shower ndani ya Meadowbrook Park

Super Middlefield grill Iddy Shah akichezesha nyama choma kwa kila mwenye kutamani nyama jana kwenye Shukurani za Sara Baby Shower iliyofanyika Meadowbrook Park Maryland nchini Marekani.

 Grill linalotoa moshi harufu nzuri ya Bongo Flaver, nyama tayari kwa kuliwa
 Stahamili joto la jikoni upate kula nyama, mrembo akiwa na subira ya kusubiri grill nyama choma chini ya mchomaji Iddy Shah subiri ziwive!
Super Middlefield grill Iddy Shah akichezesha nyama choma kwa kila mwenye kutamani nyama jana kwenye Shukurani za Sara Baby Shower iliyofanyika Meadowbrook Park Maryland nchini Marekani. 




MGOMO WA MADEREVA WATULIA, HALI YA UTULIVU YAREJEA TUNDUMA MBEYA.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gilbert Kimolo akiwasilisha hoja kwa Waziri mbele ya madereva mjini Tunduma jana. 

 Mwenyekiti wa wamiliki wa malori nchini ''DOLA'' akielezea jambo katika mkutano huo mjini Tunduma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi akiwa kwenye mkutano huo jana mjini Tunduma. 

Madereva wakiwa kwenye mkutano wa hadhara mjini Tunduma mkoani Mbeya wakati wa maridhiano ya kusitisha mgomo baada ya Waziri Omary Nundu kufika eneo hilo jana mjini Dodoma na kuwasihi waache mgomo huo Serikali inashughulikia.

KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR YAKUTANA

 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk AmaanAbeid Karume,(katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,DkAli Mohamed Shein,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,(kulia),kwa pamoja waiimba wimbo wa chama kabla ya kuanza kwa kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya halmashauri kuu ya CCM ya Zanzibar,katika ukumbi wa CCM Kisiwandui

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Amaan Abeid Karume,akiendesha kikao cha siku moja cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya Zanzibar katika ukumbi wa CCM Kisiwandui jana,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk Ali Mohamed Shein

Wiz Khalifa


Birth name Cameron Jibril Thomaz
Born September 8, 1987 (age 23)
Minot, North Dakota, United States
Origin Pittsburgh, Pennsylvania, United States
Genres Hip hop
Occupations

Rapper, Singer
Years active 2005–present
Labels Rostrum, Warner Bros., Atlantic
Associated acts Curren$y, Snoop Dogg, Big Sean, Fashawn, Mac Miller, Tinie Tempah, Rick Ross 

KUNAKO BARCLAYS PREMIER LEAGUE


Sat 13th August 2011

Blackburn v Wolves 15:00
Fulham v Aston Villa 15:00
Liverpool v Sunderland 15:00 
QPR v Bolton 15:00
Tottenham v Everton 15:00
Wigan Athletic v Norwich City 15:00
Newcastle v Arsenal 17:30
Sun 14th August 2011
Stoke City v Chelsea 13:30
WBA v Man Utd 16:00 

BREAKING NEWS: KAMANDA SIRRO AHAMISHWA MWANZA NAFASI YAKE KUSHIKWA NA BAROW LYIMO

Kamanda wa Mkoa wa Mwanza mpiganaji, Simon Sirro amehamishwa na sasa anakwenda makao makuu ya jeshi la Polisi nchini kushika nafasi ya Venance Tossi kuendesha kikosi cha Oparesheni Maalum. Mabadilio hayo yameanza sasa na nafasi yake itashikwa na Kamanda mkoa wa Tabora Barow Lyimo.